Friday, April 18, 2014

Ujumbe wa ZITTO KABWE KUELEKEA PASAKA


“Katiba ni mwafaka wa Taifa. Uandishi wa Katiba ni ujenzi wa mwafaka huo. Majadiliano ya Rasimu ya Katiba ni mchakato wa uandishi wa Katiba hiyo. Majadiliano ya upande mmoja yanaweza kuwa halali kisheria (legal legitimacy) lakini yanakosa uhalali wa kisiasa ( political legitimacy). Lazima kujenga mwafaka kwa kuhakikisha makundi yote yanashiriki katika kupata katiba ya wananchi. Asitokee wa kujidanganya kuwa kundi moja la nchi laweza kuandika katiba peke yake na ikakubaliwa na watu. Tutumie fursa ya kutafakari maisha ya Bwana Yesu katika kipindi hiki cha pasaka kutafuta na kupata mwafaka. Tunaweza”

Kutoka Facebook.

tazama video ya rais Jakaya Kikwete akielezea kuhusu Mwl, Nyerere na Mzee Karume kusemwa vibaya!


UAMUZI WA WIZARA YA FEDHA DHIDI UKAWA KUSUSIA VIKAO VYA BUNGE MAALUM LA KATIBA


Wizara ya Fedha kupitia Naibu wake Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba wametangaza uamuzi wa kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya mchakato wa Katiba vinavyoendelea Dodoma.

Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.

Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu April 10  20014 baada ya  Waziri wa Fedha kupata safari ya kikazi nchini Marekani,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato huo wa Katiba.

Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza Benki zote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance ambazo zilipelekwa Bungeni April 16 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka April 30.

Kutoka MillardAyo.Com

Msikilize Mh. Nchemba kwenye widget hii

Wednesday, April 16, 2014

DAKIKA 10 ZA PROFESA LIPUMBA ZILIZOWAONDOA BUNGENI WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA JANA!


Mfululizo wa aya 13 za Mambo muhimu aliyoyazungumza njumbe wa bunge maalum la katiba Profesa Ibrahim Haruna Lipumba akichangia mjadala wa jumla wa sura ya 1 na ya 6 ya rasimu ya katiba jana dakika 11 kabla za kuwaongoza wajumbe wa bunge hilo wa kutoka upande wa upinzani maarufu kama UKAWA kutoka nje ya bunge kwa HASIRA.

“Mimi ni muumini wa dini ya mwenyezi Mungu, lakini naafiki mapendekezo yaliyoletwa kwetu na tume ya jaji Warioba ambayo ni tume iliyoundwa na rais”.

Gazeti la Mwananchi la tarehe 14/Aprili/2014, limeandika kuwa.. nanukuu “Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu sera, uratibu na bungeni mh. William Lukuvi ameanza kampeni kanisani, kuwataka wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa serikali ya muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi”. Hii ni kauli ya waziri Lukuvi ndani ya kanisa la Methodist wakati wa sherehe ya kumsimika mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu na waziri Lukuvi alikuwa anamuwakilisha waziri mkuu.”

“Zitto Kabwe asubuhi ya leo, ameeleza vizuri kwamba tatizo letu ni usmamizi mzuri wa mapato yetu ya nchi kwamba muungano kuvunjika hauvunjiki kwa sababu ya serikali 1, 2 au 3, ni utashi wa kisiasa na haya ni maneno pia, vice chancellor wangu Pius Msekwa alishayazungumza.”

“Kama ndugu zetu waz’bar, wangekuwa wanahitaji

MCHANGO WA ZITTO KABWE KUHUSU RASIMU YA KATIBA LEO 16/04/2014


Watu wengi walikuwa na hamu ya kumsikia mbunge wa bunge maalum la katiba na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Zuberi Zitto Kabwe akichangia katika mjadala wa jumla wa rasimu ya katiba sura ya 1 na ya 6.

Hizi ni taarifa muhimu alizozungumzia mheshimiwa Kabwe katika mchango wake katika mjadala wa jumla wa rasimu ya katiba kwa sura husika leo trh. 16th / Apr / 2014.

1. Hivi sasa Serikali ya 3 imejificha ipo. Gharama ni zile zile. Sio lazima tuwe na Marais 3, hatujengi ikulu Mpya. Gharama za Wizara za Muungano zipo ndani ya Bajeti ya sasa ya Serikali mbili. Hakuna taasisi Mpya zaidi ya Tume za uwajibikaji nk.

2. Hatuhitaji kuongeza kodi, tunahitaji kuondoa ubadhirifu na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima. Tunapoteza Mapato lukuki kwenye misamaha ya kodi (theluthi ya mapato ya idara ya forodha inasamehewa, sawa na tshs 2 trilioni kwa mwaka), ukwepaji wa kodi (asilimia 5 ya Pato la Taifa inapotea, sawa na tshs 2.3 trilioni kwa mwaka ) na ubadhirifu mwingine uliokithiri. Hivyo udhibiti wa asilimia 50 tu wa misamaha ya kodi na ukwepaji kodi unaongeza mapato zaidi ya trilioni 2 ambazo Serikali ya Muungano inaweza kugawa kwa Washirika kwa miradi maalumu ya kitaifa.

3. Serikali 3 zitaweka Uwazi wa Mapato na zitaweka Uwajibikaji kwa serikali kutazamana zenyewe. Hizi za sasa zimejaa lawama sababu hakuna Uwazi. Naomba kuuliza, fedha za mapato kutoka TCRA lini zimeenda Zanzibar? Mawasiliano ni jambo la Muungano. Lini fedha za TCAA zimeenda Zanzibar? Gesi Asilia ni jambo la Muungano, hivi Zanzibar wanapata mgawo wa asilimia ngapi kutoka gesi ya Songosongo? Anga ni jambo la Muungano, fedha za chenji ya rada zimerudi, Zanzibar imepata kitabu hata kimoja? Mimi ni mwenyekiti wa PAC, najua haya ninayosema na hamtayamaliza katika S2 sababu ya confusion ya Muundo. Tatu ni Muundo unaoeleweka. Tukiamua zifanye kazi zitafanya.


Na. Godb Mhariri

WALICHOKISEMA AZAM FC KUHUSU TUHUMA YA KUNUNUA UBINGWA!

Siku 4 zimepita tangu klabu ya soka nchini inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara, Azam FC kuingia katika orodha ya klabu zilizotwaa ubingwa wa ligi kuu nchini kwa mara ya kwanza katika historia yake. Lakini kumezuka hadithi miongoni mwa wadau wa soka sehemu tofauti tofauti nchini zikiihusisha klabu ya Azam na ishu ya kuhonga wachezaji na viongozi wa timu nyingine ili washinde game zao hatimaye kutwaa ubingwa wako.

Kupitia Facebook, hii ni kauli ya Azam FC kufuatia hadithi ya kuhonga wachezaji na viongozi wa timu nyingine ili washinde michezo yao kuelekea tamati ya ligi kuu hata kutwaa ubingwa msimu huu  >>

Maneno yanayozungumzwa ni

Kauli 12 za Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu) ktk bunge la katiba trh. 15/April/2014.

Wajumbe mbalimbali kwenye bunge la katiba wameendelea kuwasha vipaza sauti vyao kuchangia, kutoa ya moyoni kwa kujadili sura ya kwanza na ya sita huku ishu ya serikali mbili au tatu ikizimiliki headlines zaidi.

Kauli za mjumbe Mh. Joseph Mbilinyi ambae pia ni mbunge wa Mbeya Mjini alizozitoa trh. 15/April/2014.

‘Wabunge Wakristo hii ni kwaresma, ni kipindi cha toba… mnatumia kipindi hiki kufanya unafiki mbele ya Wananchi mtakuja kuhukumiwa siku itakapofika, wameharibu mchakato wakati tumeshatumia mabilioni mengi ya hela’

‘Ukarabati tu wa jengo la bunge hili ili sisi tukae zimetumika BILIONI 8.2 alafu leo kwa sababu ya hotuba moja tu ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wote wamegeuka, wanaharibu kabisa tunashindwa kufanya mambo ya maana, wanaacha kupanga mkakati wa hoja wanapanga mkakati wa kuzomea, wameishiwa mikakati mpaka wanazomea kimkakati’

‘Unakutana na mbunge tena Waziri kama rafiki yangu Mwigulu Nchemba tunataniana ananiita mzee wa Maandamano mi namuita mzee wa kuteka, ananiambia wewe Sugu sijui unataka serikali tatu sijui vipi na vipi, namwambia kwani hutaki kabisa Tanganyika anasema mi nataka Tanganyika ila nataka serikali moja, sasa kama mnataka serikali moja kwa nini uibuke kwenye hoja ya serikali mbili?

‘Kuna watu ambao wanajadili vitu ambavyo

Tuesday, April 15, 2014

picha ya muundo wa serikali 3 na serikali 2 hii hapa

Picha ya juu: inaonyesha muundo wa serikali 2 wa sasa complicated na unaonyesha jinsi Serikali ya ‪#‎Tanganyika‬ ilivyojificha ndani ya Muungano. Picha ya chini: inaonyesha muundo wa serikali 3 ulio wazi na kuonyesha vyombo vinavyowajibika ‪#‎BungeKatiba‬ Serikali 3 itakuza uwazi na uwajibikaji.

via MARIA SARUNGI @facebook


Monday, April 14, 2014

KAULI ZA VIONGOZI WA KAMATI ZA BUNGE LA KATIBA 14/04/2014

Zifuatazo ni kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali wa zile kamati kwenye bunge la katiba linaloendelea pale Dodoma ambapo viongozi hawa leo April/14/2014 wameendelea kuwasilisha taarifa kutoka kwenye kamati zao..

Ni maoni ya pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo wa serikali tatu.

TUNDU LISSU: Nusu karne ya uongo iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na hakuwa na mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya Tanzania kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya muungano, nchi hii ni haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii inahitaji kuelezwa ukweli

MCHUNGAJI MTIKILA: “tulijengwa kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki hii nchi yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, swala la muungano lilikua utapeli wa kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika na Wazanzibari

MH WASSIRA: Hati ya Muungano ipo, naahidi