Wednesday, March 12, 2014

UCHAGUZI MWENYE KITI BUNGE MAALUM LA KATIBA!

Bungeni Dodoma



Zoezi la upigaji kura kumchagua mwenyekiti wa bunge maalum la katiba limalizika na zoezi la kuhesabu kura limeaza muda mfupi uliopita.

Na Gwalugano Mwakalobo

VAN PERSIE HURU KUZUNGUMZA NA KLABU NYINGINE...!!

Robin Van Persie

CR7 RONALDO.... MWANASOKA TAJIRI KULIKO ULIMWENGUNI!!!

Cristiano-Ronaldo__2719902b
Cristiano Ronaldo katika pose!!


Siku chache baada ya kutajwa na mtandao wa habari za michezo wa Goal.com kuwa mwanasoka tajiri kuliko wote Ulimwenguni, Cristiano Ronaldo amefanya kitendo ambacho kimezidi kumpatia sifa ya kuisadia wale wenye matatizo.

NI SAMWEL SITTA AU ASHIM RUNGWE KUONGOZA BUNGE MAALUM LA KATIBA...??! UCHAGUZI UMEANZA SASA!

Bungeni mjini Dodoma.

Muda mfupi uliyopita wagombeya wa nafasi ya uwenyekiti wa bunge maalum la katiba mheshimiwa Samwel John Sitta na Ashim Rungwe wamekwishajinadi na zoezi la wajumbe kupiga kura limeanza sasa.

CHANZO CHA NDEGE YA MH370 YA MALAYSIA KUPOTEA..!

Hii ni ndege ya Malaysia kabla ya kupotea.

Mkuu wa jeshi la anga la Malaysia, amekanusha madai kuwa ndege ya Malaysia iliyotoweka, ilionekana mara ya mwisho Magharibi ya rasi ya nchi hiyo, eneo ambalo ni mbali zaidi na njia iliyostahili kupita.

Tuesday, March 11, 2014

picha baada ya ajali ya basi la Hood iliyotokea Same mkoani Kilimanjaro. TUWIE RADHI KWA PICHA YOYOTE KALI



Mmoja wa waathiriwa wa ajali hiyo.
Jeshi la Polisi la uokoaji likibeba miili ya waathiriwa wa ajali hiyo.
Hivi ndivyo basi lilivyokaa baada ya ajali kutokea.

SITTA KUMBADILI PANDU KIFICHO


Samwel Sitta akipokea fomu ya kugombea nafasi ya kuwa mwenyekiti wa bunge maalum la katiba kutoka kwa ofisa wa bunge bi Lidya Mwaipyana na katikati ni mbunge wa Nzega Dk. Hamisi Kigwangala mmoja wa wajumbe wa bunge maalum la katiba.



Aliyekuwa spika wa bunge la 9 la jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samuel Sitta amechukua fomu ya kuwania nafasi ya kuwa mwenye kiti wa bunge maalum la katiba.

Katika hilo mh. Sitta  ametoa ahadi ya kusimamia haki kwa makundi yote likiwemo kundi la wajumbe mia mbili na mmoja (201) lililoteuliwa na Mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Monday, March 10, 2014

AFRIKA KUSINI KUPATA BURE MATANGAZO YA SOKA LIGI KUU UINGEREZA



Wachezaji wa klabu ya soka ya nchini Uingereza, Chelsea wakipongezana katika moja ya michezo yao ya ligi kuu.

Mashabiki wa soka nchini Afrika Kusini watapata fursa ya kutizama mechi za ligi kuu ya England bure, katika bustani mpya itakayofunguliwa mjini Johannesburg mwisho wa mwezi huu.

MATUMAINI YA KUPATIKANA KWA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA YAZIDI KUFIFIA

Juhudi za kutafuta ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliopotea usiku wa ijumaa kuamkia jumamosisaa ikiwa na abiria 227 zimeendelea kushika kasi mapema leo asubuhi katika eneo la kisiwa kilichopo nchini Vietnam ambapo inashukiwa huenda mabaki ya ndege hiyo yakapatikana katika eneo hilo.

KESI YA MCHUNGAJI MSIGWA YAHAIRISHWA

Mh.Peter Msigwa akishuka kwenye gari la  Polisi

Mbunge wa Iringa mjini Mh. Peter Msigwa amefikishwa mahakama kuu ya mkoa katika kesi yake ya kufanya vurugu kwenye kampeni ambayoimeahirishwa mpaka April 9, 2014.

Mh. Peter Msigwa anatuhumiwa kwa kosa la kumfanyia vurugu kwa kumpiga Salum Keita mjumbe wa kampeni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM ) siku ya tarehe 6 mwezi wa pili.

MBARONI KWA MAHUBIRI YA UCHOCHEZI

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera,George Mayunga
Mchungaji mmoja wa Kanisa la Chochea Moto (Emba Omulilo) ametiwa mbaroni kwa tuhuma za uchochezi na kusababisha uvunjifu wa amani katika kijiji cha Kishulo, wilaya ya Muleba, mkoani Kagera.