Aliyekuwa spika wa bunge la 9 la jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samuel Sitta amechukua fomu ya kuwania nafasi ya kuwa mwenye kiti wa bunge maalum la katiba.
Katika hilo mh. Sitta ametoa ahadi ya kusimamia haki kwa makundi yote likiwemo kundi la wajumbe mia mbili na mmoja (201) lililoteuliwa na Mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.