Saturday, March 22, 2014
MATOKEO YA MECHI KATI YA CHELSEA NA ARSENAL LIGI KUU UINGEREZA....... CHELSEA 6-0 ARSENAL

Mabao ya Timu ya Chelsea yamefungwa na Samweli Eto'o, Schurrle, Hazard akifunga kwa mkwaju wa penalti Oscar akitupia mabao mawili na Salah bao la sita na la Ushindi.
Labels:
News
TAARIFA KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA
China imeanza kuchunguza picha mpya za setilite zinazoonyesha kitu kama mabaki ya ndege kwenye eneo la kusini mwa bahari ya Hindi.
Picha hizo ni muhimu kwa ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea, maafisa wa Malaysia wanasema.
Kaimu Waziri wa Usafirishaji Hishammuddin Hussein amesoma taarifa hiyo baada ya kukabidhiwa ambapo amesema kuna kitu kama mabaki ya ndege chenye ukubwa wa mita 30 kwa 22 kilichoonekana.
Amesema serikali ya China itaendelea kutoa taarifa zaidi hapo baadae.
Ndege MH370 mali ya Shirika la ndege la Malaysia ilipotea kwenye mawasiliano ilipokuwa imeondoka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing march 8 ikiwa na abiria 239.
Labels:
News
VIJANA TANZANIA KUWEZESHWA NA IPTL
Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imeanza utekelezaji wa mpango wake wa kuwezesha miradi mbalimbali kwa vijana wa Kitanzania kuimarika kiuchumi ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya uchumi nchini.
Labels:
News
Friday, March 21, 2014
HABARI MPASUKO:ROBIN VAN PERSIE NJE WIKI 6

Mshambuliaji wa kimataifa wa Mancheater United Robin Van Persie atskuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 6 baada ya kuteguka eneo la goti.
Kwa taarifa hii van Persie anaweza kukosa michezo Man United dhidi ya Man City katika mzunguko wa ligi kuu Uingereza na Bayern Munichen katika mashindano ya Klabu bingwa Ulaya katika hatua ya robo fainali.
Van Persie aliifanikishia Man United kukata tiketi ya kwenda robo fainali kwa kuifungia mabao matatu dhidi ya Olympicos ya Ugiliki na mchezo huo kumalizika kwa Man United kushinda mabao 3-0 hata kuitupa Olympiacos nje ya michuano. Mchezo huo ulikuwa wa marudiano ambapo awali Man U ilichapwa bao 2-0 ikiwa ugenini.
Van Persie alifunga hatrick katika mchezo huo.
Labels:
News
MTANDAO WA TWITTER KUFUNGWA UTURUKI
Mtandao wa kijamii wa , Twitter, unafungwa nchini Uturuki , saa chache baada ya waziri mkuu , Recep Tayyip Erdogan, kuahidi kuuondoa .
Bwana Erdogan ambaye anakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika mkutano wa uchaguzi kuwa
Labels:
News
HABARI MPASUKO: AJALI IMETOKEA UBUNGO...!
Ajali imetokea Ubungo mataa jijini Dar Es Salaam baada ya Lori kuacha njia na kugonga magari matano.
Wangapi wamejeruhiwa na vinginevyo bado haijafahamika.... Usiache kupitia godbtz.blogspot.com
Labels:
News
KIONGOZI WA UPINZANI AACHILIWA BURUDI
Frederic Bamvuginyumvira alichiliwa kwa dhamana ili aweze kupokea matibabu |
Mahakama nchini Burundi imemwachilia kwa dhamana kiongozi mmoja mkuu wa upinzani aliyekabiliwa na kashfa za ngono pamoja na ulaji rushwa.
Wafuasi wake wanasema kuwa mashitaka hayo yalikuwa njama ya serikali kumzuia kushiriki uchaguzi mkuu kugombea urais dhidi ya Rais wa sasa Pierre Nkurunziza.
Labels:
News
Thursday, March 20, 2014
tazama picha za matukio ya Van Persie baada ya kuumia jana wakati Man U ilipoivaa Olympiacos ya Ugiriki........
Van Persie akitolewa nje ya uwanja. |
Wayne Rooney akidadisi hali ya Van Persie baada ya kuumia jana. |
Van Persie akilazwa kwenye machela baada ya kuumia. |
Labels:
News
VAN PERSIE FITI KUIVAA MAN CITY
Robin van Persie atakuwa fiti kuikabili Manchester City katika derby wiki ijayo licha ya kupata jeraha na kubebwa kwenye machela katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa ulaya uliozikutanisha Manchester United na Olympiacos Jumatano usiku.
Van Persie alikuwa shujaa katika mchezo huo baada ya kuifungia Man United mabao 3 na kuipa ushindi jumla ya mabao 3-0 (3-2 Ag.) dhidi ya Olympiacos.
Van Persie alipata jeraha dakika za mwisho za mchezo huo baada ya kukatwa na mlinzi Kostas Manolas.
Labels:
News
Wednesday, March 19, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)