Chama cha upinzani nchini India BJP kimeshinda uchaguzi mkuu kwa kupata idadi kubwa zaidi ya kura kuliko chama kingine chochote.
Kiongozi wa chama BJP Narendra Modi,amesema kuwa wananchi wajiandae kwa mambo mazuri
Matokeo ya awali yalionyesha kuwa chama hicho kimepata kura nyingi kiasi cha kuweza kutawala bila ushirikiano wowote na chama kingine.
Wafuasi wa upinzani wanasherehekeakatika makao makuu ya chama hicho.
Chama tawala cha Congress kimeshindwa baada ya kuwa mamlakani kwa miaka kumi.