Saturday, April 26, 2014

Sikiliza Na Download 'HELLO TANZANIA' by TANZANIA ALL STARs NEW!

Tanzania yatimiza miaka 50 ya Muungano

 
Jana, tarehe 26 ,Tanzania imeadhimisha miaka 50 ya Muungano tangu nchi ya Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuzaa nchi ya Tanzania.

Nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, mwaka 1964. Hii hapa historia ya Muungano huo

Historia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaanzia April 26 mwaka 1964 siku ambayo Nchi ya Jamuhuri ya Tanganyika ambayo kwa sasa ni Tanzania bara pamoja na iliyokuwa Jamuhuri ya Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja) ziliungana na kuwa nchi moja.

Hizi ni picha baadhi tu, za matukio yaliyojili katika maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa

Tsvangirai asimamishwa uongozi MDC

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change MDC kimemsimamisha kiongozi wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.

Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti, amethibitisha hilo katika mkutano wa chama hicho uliofanyika katika mji Mkuu Harare.

Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya

kama hukuitazama mechi ya Man Utd dhidi ya Norwich City, Man Utd ikiwa chini ya Ryan Giggs kama kocha na Paul Scholes kwenye benchi la ufundi. Hii ni video ya magoli yote...


Thursday, April 24, 2014

wauawa katika mlipuko Nairobi

Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.

Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.

Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi.

Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye kituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo. Alunukuliwa akisema:"kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje."

Mtaalamu wa maswala ya usalama jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.

kutoka bbc.com/swahili

Wednesday, April 23, 2014

KWA AFYA YAKO >> BANGI NI NINI.. INA ATHARI GANI..?

BAADA ya kuwepo kwa baadhi ya tafiti zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kwamba ilisaidia wagonjwa waliosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali hiyo imesababisha baadhi ya nchi kuruhusu matumizi yake.

Pamoja na mawazo ya wengi kufikiria kuwa kutokana na nchi ya Jamaica ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa watumiaji wengi ingekuwa ya kwanza kuruhusu bangi, lakini ukweli ni kwamba nchi ya Canada ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi kutumiwa kama dawa ya maradhi.

Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha kujiongezea madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.

Watafiti hao wamekwenda kinyume na wale wa kwanza kwa kusema kuwa matumizi yake yana uwezekano mkubwa wa kumletea mtumiaji magonjwa ya kupungua uzito mara kwa mara, magonjwa ya figo, ini na ugonjwa wa akili.

Watafiti waliogundua athari hizo ni

Tuesday, April 22, 2014

United Wamtimua Moyes

Meneja David Moyes amepigwa kalamu na Manchester United, klabu hicho kimetangaza Jumanne baada ya msimu wake wa kwanza kugeuka kuwa janga kubwa kwa magwiji hao wa Uingereza.
“Manchester United wanatangaza kuwa David Moyes ameondoka kwenye klabu hiki,” United walichapisha kwa anwani yao rasmi katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

“Klabu hiki kingependa kumshukuru kwa bidii, uadilifu na unyofu alioleta kwa wadhifa wake.”

Habari za kutimuliwa kwa Moyes zilijili baada ya vyombo vya habari Uingereza kutangaza kuwa utawala wa miezi 10 wa Moyes unayoyoma baada ya kumrithi gwji Sir Alex Ferguson aliyestaafu msimu jana.

Raia huyo wa Scotland 50, amejipata kwa balaa moja hadi nyingine huku United, mabingwa wa ligi ya Premier wakishuka hadi nafasi ya saba na kuchakazwa kao 2-0 na Everton Jumapili kulidhibitisha hawatafuzu kombe la mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 1995.

United wamo alama 13

MCHEZAJI AFARIKI DUNIA GABON BAADA YA KUKANYAGWA KICHWANI

Mchezaji wa klabu ya Ac Bongoville,Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke ya kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.

Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya tokeo hilo wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa

Monday, April 21, 2014

AJALI .....30 WAPOTEZA MAISHA!


Watu 30 wamepoteza maisha katika ajali ya la Luhuye lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Mwanza  baada ya kugonga mti na kupinduka wilayani Busega leo asubuhi.

Kutoka Global Publisher via +25515578