Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic
Change MDC kimemsimamisha kiongozi wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za
kidemokrasia.
Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti, amethibitisha hilo katika
mkutano wa chama hicho uliofanyika katika mji Mkuu Harare.
Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya
Waziri
Mkuu katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa kwa pamoja na Rais wa sasa
Robert Mugabe tangu mwaka 2009 hadi 2013.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia kikomo mwezi julai mwaka
2013 baada ya Rais Mugabe kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa rais na
Tsvangirai kususia uchaguzi kwa madai ya udanganyifu.
Kushindwa kwa Tsvangirai kulipunguza nguvu yake kama kiongozi
ambaye alikuwa mshindani mkuu wa Rais Mugabe.
Waangalizi wanasema ndani ya MDC kumekuwa na mgogoro wa
kiuongozi kwa miezi kadhaa.
Na. Gwalugano Mwakalobo, kutoka bbc.com/swahili