Saturday, April 26, 2014

Tanzania yatimiza miaka 50 ya Muungano

 
Jana, tarehe 26 ,Tanzania imeadhimisha miaka 50 ya Muungano tangu nchi ya Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuzaa nchi ya Tanzania.

Nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, mwaka 1964. Hii hapa historia ya Muungano huo

Historia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaanzia April 26 mwaka 1964 siku ambayo Nchi ya Jamuhuri ya Tanganyika ambayo kwa sasa ni Tanzania bara pamoja na iliyokuwa Jamuhuri ya Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja) ziliungana na kuwa nchi moja.

Hizi ni picha baadhi tu, za matukio yaliyojili katika maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar;
Amiri Jeshi Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Raid Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) sambamba na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) wakiingia katika uwanja wa taifa wa Uhuru tayari kushereheka maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.



Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya muungano.



Vilevile Mkomandoo walipata fursa ya kufanya vitu vyao. Hapa wakipasua matofali vichwa na ngumi.