Monday, May 5, 2014

KIONGOZI WA MAANDAMANO ATIWA MBARONI NIGERIA

Mwanaharakati mwanamke aliyekuwa akiongoza maandamano nchini Nigeria kushinikiza serikali ya nchi hiyo kuwaokoa wasichana 200 waliotekwa hivi karibuni ametiwa mbaroni na polisi kwa amri ya mke wa Rais wa nchi hiyo.
Naomi Mutah Nyadar alikuwa miongoni wanawake waliohudhuria mkutano ulioitishwa na ma mke wa rais Patience Jonathan na baadae mwanaharakati huyo alipelekwa kituo cha polisi.