Hii leo Manchester United imeicharua mabao 4-1 Aston Villa katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ambapo Manchester United walikuwa wenyeji wa mchezo huo katika uwanja wao wa Old Trafford.
Aston Villa alikuwa wa kwanza kupata bao la kwanza la kuongoza kupitia nyota wake Westwood katika dakika ya 13 ya kipindi cha kwanza.
Manchester United ilijibu mashambulizi kwa kusawazisha bao la Aston Villa kupitia mshambuliaji wake Wayne Rooney dakika ya 20 na kuongeza bao jingine la kuongoza dakika ya 45 kipindi cha kwanza. Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata katika dakika ya 57 na Chicharito kufunga hesabu dakika ya 90.
Haya ni matokeo ya mchezo mingine ya leo ya ligi kuu ya Uingereza:
Stoke City 1 - 0 Hull City,
Swansea City 3 - 0 Norwich City,
Southampton 4 - 0 Newcastle United,
West Bromwich Albion 3 - 3 Cardiff
City,
Crystal Palace 1 - 0 Chelsea na
Arsenal 1 – 1 Manchester City