Tuesday, April 22, 2014

MCHEZAJI AFARIKI DUNIA GABON BAADA YA KUKANYAGWA KICHWANI

Mchezaji wa klabu ya Ac Bongoville,Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke ya kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.

Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya tokeo hilo wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa
amelisimamisha kombora lililopigwa langoni mwake, lakini mshambulizi alipoteza mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani.

Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa Bongoville ambalo liko umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.

"Ni vigumu sana kushuhudia hali hii ya uchungu ,'' ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.

kutoka bbc.com/swahili