Tuesday, April 22, 2014

United Wamtimua Moyes

Meneja David Moyes amepigwa kalamu na Manchester United, klabu hicho kimetangaza Jumanne baada ya msimu wake wa kwanza kugeuka kuwa janga kubwa kwa magwiji hao wa Uingereza.
“Manchester United wanatangaza kuwa David Moyes ameondoka kwenye klabu hiki,” United walichapisha kwa anwani yao rasmi katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

“Klabu hiki kingependa kumshukuru kwa bidii, uadilifu na unyofu alioleta kwa wadhifa wake.”

Habari za kutimuliwa kwa Moyes zilijili baada ya vyombo vya habari Uingereza kutangaza kuwa utawala wa miezi 10 wa Moyes unayoyoma baada ya kumrithi gwji Sir Alex Ferguson aliyestaafu msimu jana.

Raia huyo wa Scotland 50, amejipata kwa balaa moja hadi nyingine huku United, mabingwa wa ligi ya Premier wakishuka hadi nafasi ya saba na kuchakazwa kao 2-0 na Everton Jumapili kulidhibitisha hawatafuzu kombe la mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 1995.

United wamo alama 13
nyuma ya nafasi ya nne na 23 nyuma ya watanashari wao Liverpool wanaopigiwa upatu kuwaridhi kama mabingwa wa Premier ikisalia mechi nne muhula huu kwisha.

Kulingana na duru, afisa mkuu mtendaji wa United, Ed Woodward, aliarifu Moyes binafsi uamuzi wa kumpiga kalamu katika makao yao ya Carrington Jumanne asubuhi.

Mkongwe Ryan Giggs na mwenzake Nicky Butt wanatarajiwa kuchukua hatamu za uongozi kwa muda na kuongoza United dhidi ya Norwich City Jumamosi huku miamba hao wakisaka mrithi ambaye atarejesha hadhi yao.


Louis van Gaal, kocha wa Uholanzi, amepigiwa upatu na wadau kuchukua wadhifa huo huku Jurgen Klopp (Borrusia Dortmund), Diego Simeone (Atletico Madrid) na Giggs wakitajwa kama wengine wanaowazwa na bodi ya klabu hicho.

kutoka Supersport.com