
Mshambuliaji wa kimataifa wa Mancheater United Robin Van Persie atskuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 6 baada ya kuteguka eneo la goti.
Kwa taarifa hii van Persie anaweza kukosa michezo Man United dhidi ya Man City katika mzunguko wa ligi kuu Uingereza na Bayern Munichen katika mashindano ya Klabu bingwa Ulaya katika hatua ya robo fainali.
Van Persie aliifanikishia Man United kukata tiketi ya kwenda robo fainali kwa kuifungia mabao matatu dhidi ya Olympicos ya Ugiliki na mchezo huo kumalizika kwa Man United kushinda mabao 3-0 hata kuitupa Olympiacos nje ya michuano. Mchezo huo ulikuwa wa marudiano ambapo awali Man U ilichapwa bao 2-0 ikiwa ugenini.
Van Persie alifunga hatrick katika mchezo huo.