Robin van Persie atakuwa fiti kuikabili Manchester City katika derby wiki ijayo licha ya kupata jeraha na kubebwa kwenye machela katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa ulaya uliozikutanisha Manchester United na Olympiacos Jumatano usiku.
Van Persie alikuwa shujaa katika mchezo huo baada ya kuifungia Man United mabao 3 na kuipa ushindi jumla ya mabao 3-0 (3-2 Ag.) dhidi ya Olympiacos.
Van Persie alipata jeraha dakika za mwisho za mchezo huo baada ya kukatwa na mlinzi Kostas Manolas.