Wajumbe mbalimbali kwenye bunge la
katiba wameendelea kuwasha vipaza sauti vyao kuchangia, kutoa ya moyoni kwa
kujadili sura ya kwanza na ya sita huku ishu ya serikali mbili au tatu
ikizimiliki headlines zaidi.
Kauli za mjumbe Mh. Joseph Mbilinyi
ambae pia ni mbunge wa Mbeya Mjini alizozitoa trh. 15/April/2014.
‘Wabunge Wakristo hii ni kwaresma,
ni kipindi cha toba… mnatumia kipindi hiki kufanya unafiki mbele ya Wananchi
mtakuja kuhukumiwa siku itakapofika, wameharibu mchakato wakati tumeshatumia
mabilioni mengi ya hela’
‘Ukarabati tu wa jengo la bunge hili
ili sisi tukae zimetumika BILIONI 8.2 alafu leo kwa sababu ya hotuba moja tu ya
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wote wamegeuka, wanaharibu kabisa tunashindwa
kufanya mambo ya maana, wanaacha kupanga mkakati wa hoja wanapanga mkakati wa
kuzomea, wameishiwa mikakati mpaka wanazomea kimkakati’
‘Unakutana na mbunge tena Waziri
kama rafiki yangu Mwigulu Nchemba tunataniana ananiita mzee wa Maandamano mi
namuita mzee wa kuteka, ananiambia wewe Sugu sijui unataka serikali tatu sijui
vipi na vipi, namwambia kwani hutaki kabisa Tanganyika anasema mi nataka
Tanganyika ila nataka serikali moja, sasa kama mnataka serikali moja kwa nini
uibuke kwenye hoja ya serikali mbili?
‘Kuna watu ambao wanajadili vitu
ambavyo
hawaviamini na havipo kwenye mioyo yao na hao watu wanadhamana kwenye
uongozi wa taifa hili na hii ni hatari’
‘Tuko kwenye nafasi nzuri sana ya
kujadili hili swala, tulijadili wakati tunaheshimiana kuliko siku tuje
kulazimisha mabadiliko ambayo hatukuyapanga, tusifikie sehemu Wazanzibari hao
wanaosemwa elfu sitini ndio waingie barabarani na jeshi’
‘Mwenyekiti alikuja hapa akatutisha
oooh sijui serikali tatu jeshi, Mwanajeshi atakuja atachukua nchi… Mwenyekiti
mwenyewe alikua ni Mwanajeshi akavua uniform, Nyerere aliposema vueni uniform
akavua na leo ni rais, kuna ubaya gani Mwanajeshi akitawala kama ana akili?
hakuna ubaya, wanajeshi ni ndugu zetu’
‘Hakuna tatizo lolote siku
Mwanajeshi akija kuwa Rais kwa sababu tunae Mwanajeshi Rais Kikwete na
anaendelea tu, asiweke vikwazo kwa Wanajeshi wengine ambao watakua na tija kwa
taifa hili’
‘Wanasema serikali tatu gharama,
hivi kama gharama inaongezeka alafu tija inaongezeka kuna tatizo gani? ukifanya
biashara rejareja ukitaka kuwa mkubwa ni lazima uongeze mtaji, kama huu mfumo
wa serikali mbili umeshindwa kutuondolea matatizo mwengine anasema Znz wana
hiki wana kile, mbona hamsemi kama mpaka umeme tunawalipia?? lakini sisi huku
tunalia’
‘Tuna serikali mbili na hakuna
aliesimama hapa akasema serikali mbili gharama zake zipi, Wizara ngapi hapa
zinapanga majengo kila siku yanatolewa furniture? serikali tatu gharama
against what? against tija? against maendeleo? against kwenda mbele?
‘Sababu akili yenu ni fedha ndio
maana mnaangalia faida kwamba ni fedha tu, hamuangalii faida nyingine za
kijamii ambazo zitaleta tija kwa taifa hili’
‘Kuna hawa ndugu zangu viongozi wa
dini, tunasema hivi mara nyingi viongozi wa dini wamekosea walipochagua kuwa
upande wa dola dhidi ya matakwa ya nchi, hii imetokea mfano ni Padri wa Rwanda,
leo hii yukwapi? kwa hiyo viongozi wa dini wawe makini wanavyoangazia haya
maswala’
‘Mungu ibariki Tanganyika, Mungu
ibariki Zanzibar , Mungu bariki mchakato huu wa shirikisho la Zanzibar na
Tanganyika, acheni kutupiga mkwara eti tutagawana mbao… ni heri kugawana mbao
kuliko kwenda kuzinguana huko mbele ya safari’
kutoka TBC na MILLARDAYO.COM