Wednesday, April 16, 2014

WALICHOKISEMA AZAM FC KUHUSU TUHUMA YA KUNUNUA UBINGWA!

Siku 4 zimepita tangu klabu ya soka nchini inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara, Azam FC kuingia katika orodha ya klabu zilizotwaa ubingwa wa ligi kuu nchini kwa mara ya kwanza katika historia yake. Lakini kumezuka hadithi miongoni mwa wadau wa soka sehemu tofauti tofauti nchini zikiihusisha klabu ya Azam na ishu ya kuhonga wachezaji na viongozi wa timu nyingine ili washinde game zao hatimaye kutwaa ubingwa wako.

Kupitia Facebook, hii ni kauli ya Azam FC kufuatia hadithi ya kuhonga wachezaji na viongozi wa timu nyingine ili washinde michezo yao kuelekea tamati ya ligi kuu hata kutwaa ubingwa msimu huu  >>

Maneno yanayozungumzwa ni
porojo Baada ya Azam Fc kupata mafanikio ya kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam Fc ilipata nafasi ya pili mara Mbili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara haikuwai kusemwa imenunua leo iweje imekuwa Bingwa isemwe imenunua.

John Bocco ameweka Historia Baada ya Kufunga Goli la Ushindi ktk Mechi ya Mwisho ya Ligi Daraja la kwanza na Kuipandisha Azam Fc kucheza Ligi kuu ya Tanzania Bara, na leo Hii Tumeshuhudia John Bocco ameweka Historia ya Kufunga Goli la Ushindi na Kuipa Timu ya Azam Fc Ubingwa kwa Mara ya kwanza Tangu ilipopanda Daraja kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara kwa Msimu 2013/2014 na kucheza Bila kupoteza hata mechi Moja.

Hatuto puuzia mechi ya mwisho Dhidi ya JKT Ruvu Tutacheza kama mechi nyingine Tulivyocheza Tunahitaji kuweka Historia ya Kutokupoteza hata Mechi Moja kwa Msimu Huu JKT Ruvu wajiandae kwa Kichapo wakati Tukiwa Tunakabidhiwa Kombe letu la Msimu Huu

Baadhi ya Maneno ambayo Makocha wanazungumza Sio Mazuri wao kama wataalam hawatakiwi kujihusisha katika Propaganda ambazo baadhi ya watu wanaziendeleza.


Na. Gwalugano ‘Godb’ Mwakalobo