Watu
wengi walikuwa na hamu ya kumsikia mbunge wa bunge maalum la katiba na bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Zuberi Zitto Kabwe akichangia katika
mjadala wa jumla wa rasimu ya katiba sura ya 1 na ya 6.
Hizi ni taarifa muhimu alizozungumzia mheshimiwa Kabwe
katika mchango wake katika mjadala wa jumla wa rasimu ya katiba kwa sura husika
leo trh. 16th / Apr / 2014.
1.
Hivi sasa Serikali ya 3 imejificha ipo.
Gharama ni zile zile. Sio lazima tuwe na
Marais 3, hatujengi ikulu Mpya. Gharama za Wizara za Muungano zipo ndani ya
Bajeti ya sasa ya Serikali mbili. Hakuna taasisi Mpya zaidi ya Tume za
uwajibikaji nk.
2.
Hatuhitaji kuongeza kodi, tunahitaji
kuondoa ubadhirifu na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima. Tunapoteza Mapato
lukuki kwenye misamaha ya kodi (theluthi ya mapato ya idara ya forodha inasamehewa, sawa na tshs 2 trilioni kwa mwaka), ukwepaji
wa kodi (asilimia 5 ya Pato la Taifa
inapotea, sawa na tshs 2.3 trilioni kwa mwaka ) na ubadhirifu mwingine
uliokithiri. Hivyo udhibiti wa asilimia 50 tu wa misamaha ya kodi na ukwepaji
kodi unaongeza mapato zaidi ya trilioni 2 ambazo Serikali ya Muungano inaweza
kugawa kwa Washirika kwa miradi maalumu ya kitaifa.
3. Serikali 3 zitaweka Uwazi wa Mapato na zitaweka Uwajibikaji kwa
serikali kutazamana zenyewe. Hizi za sasa zimejaa lawama sababu hakuna
Uwazi. Naomba kuuliza, fedha za mapato
kutoka TCRA lini zimeenda Zanzibar? Mawasiliano ni jambo la Muungano. Lini fedha za TCAA zimeenda Zanzibar?
Gesi Asilia ni jambo la Muungano, hivi Zanzibar wanapata mgawo wa asilimia
ngapi kutoka gesi ya Songosongo? Anga ni jambo la Muungano, fedha za chenji ya
rada zimerudi, Zanzibar imepata kitabu hata kimoja? Mimi ni mwenyekiti wa PAC,
najua haya ninayosema na hamtayamaliza katika S2 sababu ya confusion ya Muundo.
Tatu ni Muundo unaoeleweka. Tukiamua zifanye kazi zitafanya.
Na. Godb Mhariri