Monday, April 14, 2014

KAULI ZA VIONGOZI WA KAMATI ZA BUNGE LA KATIBA 14/04/2014

Zifuatazo ni kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali wa zile kamati kwenye bunge la katiba linaloendelea pale Dodoma ambapo viongozi hawa leo April/14/2014 wameendelea kuwasilisha taarifa kutoka kwenye kamati zao..

Ni maoni ya pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo wa serikali tatu.

TUNDU LISSU: Nusu karne ya uongo iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na hakuwa na mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya Tanzania kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya muungano, nchi hii ni haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii inahitaji kuelezwa ukweli

MCHUNGAJI MTIKILA: “tulijengwa kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa kubariki hii nchi yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, swala la muungano lilikua utapeli wa kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika na Wazanzibari

MH WASSIRA: Hati ya Muungano ipo, naahidi
kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa Mwenyekiti ndani ya siku mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni kutaka kuvunja muungano, je tume ingeyaleta? serikali 3 italeta mgongano

MH WASSIRA: Katiba ya Z'bar ndio itabakia kuwa sheria kuu kwa Z'bar kwa mambo yasiyokua ya muungano, tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata matatizo, itapunguzia Wazanzibari fursa

ISMAIL JUSSA: Hoja za historia kwamba tulikua vipi haziwezi kulibakisha taifa katika mgando, ukiangalia katiba ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua Tanganyika na kuwepo makamu wawili wa Rais

ISMAIL JUSSA: Mkataba wa muungano haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha kilichopo ndani, ajabu bunge limefanya, tunapokua Znz tunasema mengine tukija huku tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu

ISMAIL JUSSA: “Z'bar tumeachwa watupu, tumechoka na hatukubali tena, ktk mfumo wa serikali mbili Z'bar haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali kuendelea nao

ISMAIL JUSSA: Kama kuna nia njema kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni Rais wa Z’bar kuondolewa kuwa makamu wa Rais


Chanzo MILLARDAYO.COM na TBCtv