Wizara
ya Fedha kupitia Naibu wake Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba wametangaza
uamuzi wa kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya mchakato wa Katiba
vinavyoendelea Dodoma.
Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa
Bunge la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai
wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa
anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu April 10 20014 baada ya Waziri
wa Fedha kupata safari ya kikazi nchini Marekani,amefuta Malipo ya wabunge
waliosusia Mchakato huo wa Katiba.
Kutoka MillardAyo.Com
Msikilize Mh. Nchemba kwenye widget hii