Kikao cha bunge maalum la katiba kimeshindwa kuendelea leo hii
baada ya kukatika kwa matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni ya Taifa
TBC na kulalamikiwa na wajumbe 'kundi la wachache' wanaotaka serikali tatu,
ambapo taarifa yao ya kamati namba nne ndio ilikuwa ikiwasilishwa.
Mwenyekiti wa bunge hilo maalum la katiba mh. Samwel Sitta alisema
lengo la bunge kuingia mkataba na TBC ni
kutaka Wananchi waone kila
kinachotokea ndani ya bunge ili kuwezesha kupatikana kwa katiba bora ambayo
Wananchi wataipigia kura ili kutoa maamuzi ndio maana akatoa tangazo la
kusitisha kikao.
Alisema "kwa sababu yoyote ile hatuwezi kuendelea, natoa
maelezo tusikilizane… natoa maelekezo kwa katibu kuangalia muda ilipozimika na
Mh. Tundu Lissu alikwa anaongea ili Jumatatu tutakapo rejea nimpe Lissu nafasi
ya kwanza kuweza kumalizia"
Matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa tbc
yalikata ghafla wakati mh. Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya waliyowachache
katika kamati yao.
Lakini nje ya ukumbi wa bunge katibu wa baraza la habari Tanzania
(MCT) ambaye pia ni mjumbe wa bunge hilo Kajubi Mukajanga akatoa tamko kwa
kusema "ni jambo la kusikitisha na la aibu, naongea kama Mjumbe na
pia Katibu wa baraza la habari… kitendo kilichofanyika leo mpaka hapo
tutakapo pata ushahidi kwamba kweli kulikua na tatizo la kimitambo"
"Ni kitendo cha aibu na kuhujumu tasnia ya habari,
haiwezekani mawazo haya yakarushwa…… mawazo haya yasirushwe kwa sababu watu
waliopewa majukumu ya kusimamia kituo cha taifa (TBC) wanadhani kwamba
hawayapendi mawazo hayo" aliongeza Mukajanga.
CHANZO MILLARDAYO.COM