Saturday, March 8, 2014

MAN UNITED YAIMALIZA WESTBROMWICH BPL!!!!

Na. Gerald Nyang'ali
Ingali katika wakati mgumu klabu ya soka Manchester United imemchapa WestBromwich mabao 3-0 katika mtanange wa ligi kuu Barclays Uingereza.

Mabao ya Manchester yalitiwa kambani na Phil Jones, Rooney na Welbeck aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya mholanzi Robin Van Persie
.



Jones aliipatia Manchester bao la kwanza katika dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza akimaliza faulo maridadi iliyochongwa na Van Persie, bao la pili likafungwa na mshambuliaji Wayne Rooney kipindi cha pili na hesabu kufungwa na Dan Welbeck dakika ya 83 ya mchezo huo.

Westbromwich walikuwa wenyeji wa mchezo huo wakimkaribisha Man United katika dimba la The Hawthorns.

Man United wanashika nafasi ya sita kwa sasa kufuatia matokeo hayo huku Everton ikiwa na mchezo mmoja mkononi iko katika nafasi ya saba kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungana.