Tangu TFF kusema inatafuta kocha mpya atakayerithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen, BIN ZUBEIRY imekuwa ikifuatilia kwa undani mwalimu mpya wa Stars atakuwa nani na sasa inaibuka na jibu ni Mart Nooij.
Tayari Nooij ambaye kwa sasa ni kocha wa St George ya Ethiopia amekwishasaini Mkataba wa miaka miwili na TFF na atakuja nchini mwishoni mwa mwezi huu.
![]() |
| Kocha mpya wa taifa
stars ni Mholanzi ambaye anafahamika kwa jina la Martinus Ignatius
anayetarajiwa kutambulishwarasmi march 24 mwaka huu na rais wa TFFJamal Malinzi |
