Sunday, March 16, 2014

Hali ya Man utd imezidi kuwa shakani kufuatia kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Liverpool katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya chini Uingereza /EPL.

Manchester Utd akiwa mwenyeji wa mchezo huo kunako Old Traffold, amekubali kichapo cha mabao 3-0, mabao hayo ya Liverpool yamefungwa na Stevne Gerald maarufu mr. Liverpool na Luiz Suarez.

Gerald aliiandikia Liverpool bao la kwanza kwa mkwaju wa penati 35' ya kipindi cha kwanza na lingine la pili 46' kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati halikadhalika na bao la tatu likafungwa na Suarez 84' kipindi cha pili.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Mark Clatternburg, beki wa kati Nemanja Vidic alizawadiwa kadi nyekundu na kuondolewa mchezoni baada kumfanyia madhambi straika Daniel Sturridge ndani ya eneo la hatari na kusababisha penati ambayo hata hivyo Gerald aliipoteza na kupishana na hatrick!